Bofya hapa kusoma taarifa ya utafiti iliyo kwa lugha ya kiingereza
Utafiti
Udhibiti Wa Bidhaa Bandia: Utafiti Kifani Wa Chumvi Yenye Madini Joto
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya utafiti huu kwa lengo la kutoa ushauri wa namna bora ya kuimarisha mfumo wa usimamizi (monitoring) na utekelezaji wa sheria na kanuni za chumvi yenye madini joto kwa mamlaka zinazohusika katika mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi kwa matumizi ya binadamu na wanyama. Bonyeza Kusoma Zaidi.
MIANYA YA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifanya utafiti kwa lengo la kutoa ushauri kwa Mamlaka zinazohusika juu ya namna bora ya kudhibiti vitendo vya rushwa katika Chaguzi nchini. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: (i) Kubaini mianya ya rushwa katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014; (ii) Kutathmini uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa; (iii) Kuainisha vitendo vya rushwa vilivyojitokeza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014; na (iv) Kushauri namna ya kuziba mianya ya rushwa itakayobainika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Soma Zaidi