JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

Kampeni za uelimishaji

UELIMISHAJI KUPITIA KAMPENI MBALIMBALI

Rushwa ni tatizo ambalo athari zake zinamgusa kila mwananchi. Tatizo hili linasababisha jamii kukosa imani na Serikali yao, amani baina ya wanajamii, kujenga matabaka ya walionacho na wasiokuwa nacho. Vilevile rushwa imekuwa chanzo cha kudhoofisha huduma zinazotolewa katika jamii kitaifa na kimataifa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki Moon alisema wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Rushwa, Desemba 9, 2013, “Kila mmoja, serikali mbalimbali na jamii kwa ujumla zinatakiwa kupambana na rushwa ili kuifanya dunia mahali salama pa kuishi”.

Kupitia wito huo, TAKUKURU inatumia njia na kampeni mbalimbali kufikisha elimu ya mapambano dhidi ya rushwa ili kuifanya Tanzania mahali pazuri na salama pa kuishi.

1.0 KAMPENI YA LONGA NASI YA MWAKA 2016

Ili kutimiza jukumu hili linalotajwa katika kifungu cha 7 (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007, inaendesha Kampeni ya Longa nasi ya mwaka 2016 amapo imelenga umma kushiriki zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa kuzidi hapo nyuma. Hii inamtaka kila mwananchi sehemu alipo aweze kushiriki kutoa maoni, ushauri na taarifa za vitendo vya rushwa bila kuchukua muda mrefu. TAKUKURU inatambua kuwa kila mwananchi akielimika na kutambua anawajibika kuzuia vitendo vya rushwa na kutoa taarifa hizo, rushwa inaweza kutokomezwa nchini kupitia Kampeni ya Longa nasi au Longa na TAKUKURU.

   1.0       TAARIFA YA KAMPENI YA LONGA NASI

Kampeni ya Longa nasi ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mei 24, 2016 katika viwanja vya Mwembeyanga jijini, Dar es Salaam ambapo alisema dhamira ya Serikali kuwa haiko tayari kuona vitendo vya rushwa vinaendelea katika jamii na ndiyo maana imezinduliwa kampeni hiI. Uelimishaji kupitia Longa nasini wa kitaifa ambapo inaendelea nchi nzima katika mikoa na wilaya zake kwa kuratibiwa na TAKUKURU.

Wakati wa uzinduzi wa kampeni hii, wananchi, viongozi mbalimbali na wadau wa kampuni za mawasiliano walishiriki za TTCL, Tigo, Airtel, Zantel, Halotel na Vodacom. Mojawapo ya viongozi waliohudhuria ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumi na Utawala Bora., Mhe. Angela Kairuki.

Mhe. Kairuku alisema kuwa kampeni ya Longa Nasi itumike kuwa mwarobaini dhdi ya wala rushwa katika jamii yetu. Kila mmoja awe jasiri kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mtaa wake, kijiji au katika eneo linalomzunguka.Tujenge tabia ya kuhoji pale mazingira yanapoonekana kutia wasiwasi kuashiria vitendo vya rushwa.

Alieleza kuwa wananchi, wakumbuke kuwa wakifumbia macho vitendo vya rushwa taifa litaangamia. Serikali itashindwa kutoa huduma bora kwa wananchi wake, hivyo kuhatarisha usalama na amani ya taifa. Ili kukabiliana na tatizo hili kila mmoja awe balozi wa mapambano dhidi ya rushwa na kutanguliza uzalendo mbele.

 1.1 MATARAJIO YA KAMPENI

Kampeni hii inaamsha ari ya wananchi kushiriki mapambano dhidi ya rushwa na kuwahamasisha kutoa taarifa za rushwa zitakazowezesha kuchukuliwa hatua stahili za kisheria dhidi ya wala rushwa. Kampeni ya Longa nasi inatumia maigizo, machapisho na ujumbe wake katika kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa.

Inatarajiwa kuwa utekelezaji wa kampeni ya ‘LONGA NASI’ utaleta manufaa yafuatayo:

  1. Uelewa wa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa utaongezeka. Hali hii itasaidia wao kwa wao kuelimishana na hivyo kuzuia vitendo vya rushwa.
  2. Wananchi watajengewa ujasiri zaidi ili kuongeza ushiriki wao katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa, kutoa mrejesho wa kero zilizotatuliwa na kutoa ushahidi mahakamani.
  3. Huduma kwa umma zitaboreka kwa fedha zinazopangwa kutoa huduma hizo kutumika kadiri ya mipango iliyoidhinishwa.
  4. Watumishi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wataripotiwa zaidi na kuchukuliwa hatua za kisheria jambo litakalowaogofya wengine (deterrence effect) kuomba na kupokea rushwa au kufuja fedha na mali za umma.
  5. Wananchi watapata huduma bora pasipo kudaiwa au kutoa rushwa.

TAKUKURU itajijengea taswira chanya katika jamii kuwa ni kimbilio la wananchi wanaodhulumiwa haki au stahiki zao kwa vitendo vya rushwa.

  1. TAKUKURU itapata mrejesho kutoka kwa umma wa jinsi unavyoichukulia Taasisi na utekelezaji wa majukumu yake kisheria.

1.2 HALI YA KAMPENI HIVI SASA

Tangu kuzinduliwa kwa  kampeni ya Longa nasi Mei, 2016, tayari inaendelea nchi nzima kwa hatua mbalimbali za kuhamasisha wananchi kutoa taarifa  za vitendo vya rushwa, maoni na mapendekezo namna ya kupambana na vitendo vya rushwa.Kwa  Dar es Salaam imefanyika katika mikoa ya Ilala, Kinondoni na Temeke ambapo taarifa za vitendo vya rushwa 65,976zimeshapokelewa na kufanyiwa kazi. Hizi zinajumuisha kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia 113,*113#. Haya ni matokeo chanya ya wananchi wanaoshiriki kupambana na rushwa kupitia kampeni ya Longa nasi.