JIVUNIE UNAPOSEMA ‘SIRUBUNIKI KWA RUSHWA.’

 

 

Sidebar

Klabu za Wapinga Rushwa

 1. USHIRIKI WA VIJANA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.

TAKUKURU imekuwa ikishirikisha vijana katika mapambano dhidi ya rushwa kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha kwa njia ya semina, matamasha ya sanaa, midahalo, Mikutano ya Hadhara, Uchoraji Katuni, Utunzi wa Insha au Mashairi na Mijadala ya wazi. Pia vijana wamekuwa wakishiriki kwenye vipindi vya redio na televisheni.

 1. UANZISHWAJI WA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA.

Mnamo mwezi Mei, 2007 TAKUKURU ilianzisha kampeni ya kufungua klabu za wapinga rushwa katika shule za sekondari Tanzania Bara ambapo Mkurugenzi Mkuu alizindua klabu ya wapinga rushwa shule ya Sekondari Makongo kama ishara ya kuanza rasmi kampeni hii.

Hata hivyo, ujenzi wa maadili unatakiwa kuanzia ngazi ya msingi, hivyo Mnamo mwezi Julai , 2013 TAKUKURU iliona ni vema klabu hizi zikaanzishwa katika shule za msingi. Hii itasaidia kuleta mabadiliko ya kijamii hususani katika kubadili mtazamo wa jamii kutoka kwenye mtazamo kuwa rushwa ni sehemu ya utamaduni na kuiona rushwa kuwa ni tatizo la kitaifa lisilotakiwa kuvumiliwa kwa namna yoyote. Ili rasilimali hii iweze kutumika vizuri zaidi, kuna umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza klabu katika shule za msingi.

 

 1. TAKWIMU ZA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA.

IDADI YA KLABU ZA WAPINGA RUSHWA ZILIZOFUNGULIWA TANGU MEI 2007 HADI JUNI 2016

MWAKA S/MSINGI SEKONDARI VYUO JUMLA
  Idadi Wanachama Idadi Wanachama Idadi Wanachama Idadi Wanachama
2007     1284 65,518     1284 65,518
2008     347 22,439     347 22,439
2009     2030 147,358     2030 147,358
2010     130 8,208     130 8,208
2011     100 7,382     100 7,382
2012     93 11,833 65 4158 158 15,991
2013 1,906 126,340 76 12,288 6 4,300 1,988 142,928
2014 880 80322 51 4913 11 1018 942 86,253
2015 216 23450 47 4118 26 2168 289 29,736
2016 509 29392 11 565 0 0 520 29,957
JUMLA 3,511 259,504 4,169 284,622 108 11,644 7,788 555,770
 1. MCHANGO WA VIJANA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
 • Kueneza ujumbe wa kutokomeza rushwa kwa jamii kwa kuelimisha wengine kuhusu rushwa, athari zake na namna ya kupambana nayo.
 • Kushiriki katika kazi mbalimbali za uelimishaji zinaandaliwa na kuendeshwa kwa ajili ya kuwajengea vijana ufahamu na ujasiri wa kupambana na rushwa.
 • Kukataa kujihusisha na vitendo vya rushwa ikiwemo kutoa au kupokea rushwa.
 • Kutoa taarifa za  vitendo vya rushwa katika ofisi za  TAKUKURU zilizo karibu   au kwa kupiga simu ya bure  namba 113 au kwa vyombo vingine vya dola na viongozi wanaohusika. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 39 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007
 • Kujifunza na kuelewa haki na wajibu wa kila mwananchi pamoja na kuijua katiba ya nchi.
 • Kuzingatia maadili na kuwa mzalendo kwakuwa mtu anapoipenda nchi yake kwa dhati atakuwa mstari wa mbele kutetea haki na kuipigania kwa namna yoyote.
 • Kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na vyombo vingine vya dola na kuwa tayari kutoa ushahidi wa vitendo vya rushwa kwakuwa mara nyingi TAKUKURU imekuwa ikishindwa kufikia malengo kutokana na wananchi kutotaka kutoa ushirikiano.