KIKAO KAZI – DODOMA

KIKAO KAZI – DODOMA

Kikao kati ya watumishi wa TAKUKURU Dodoma na timu ya Mheshimiwa Rais ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai, kimefanyika jijini...

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2023 – DODOMA

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2023 – DODOMA

 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye, amewaongoza wanawake wa TAKUKURU MakaoMakuu na wale wa Ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, kutembelea wahitaji (watoto wanaoishi katika mazingira magumu, yatima pamoja na wazee),ambao wanalelewa katika Kituo cha Mtakatifu Theresa - Shirika la Upendo kilichopo Hombolo jijini Dodoma, Machi 8, 2023.

TUME YA HAKI JINAI, YAFIKA WILAYANI ARUMERU

TUME YA HAKI JINAI, YAFIKA WILAYANI ARUMERU

 Wajumbe wa Tume iliyoundwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kupokea maoni ya kuboresha utendaji wa Taasisi za Haki Jinai nchini imefika na kuzungumza na Wakuu wa TAASISI za HakiJinai Wilayani Arumeru, Maaskari na Wananchi wa Kijiji cha Ngarasero, USA RIVER. Mwenyekiti wa Tume, JAJI Mstaafu Othman Chande (wa tatukutoka kushoto) aliwataka wananchi na Viongozi wa Taasisi za Haki Jinai, kuelezea kwa uhuru na bila kificho, CHANGAMOTO zozote wanazoziona wakatiwa kutoa au kupata haki kwenye vyombo vya dola. Akifafanua, maana ya HAKI JINAI, alieleza ya kwamba, "Mnyororo wa haki huanzia wakati uhalifuunafanyika, ukamataji, upelelezi, kufikishwa mahakamani,  kutolewa kwa hukumu, kufungwa gerezeni na kutoka gerezani hadi muda wa kurejea kwenyejamii"  Mkuu wa TAKUKURU (W) Arumeru Bw Deogratius Mtui ni miingoni mwa waliotoa maoni Yao. TAKUKURU ARUMERU Machi 3, 2023.

USHIRIKIANO NA WADAU

USHIRIKIANO NA WADAU

 " TAKUKURU inaendelea kushirikiana na wadau kama Women Fund Tanzania Trust - WFT, katika mapambano dhidi ya rushwaikiwemo Rushwa ya Ngono...". Haya yamesemwa na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Bi. Sabina Seja katika Kongamano la kuadhimisha miaka 15 ya WomenFund Tanzania Trust, linaloendelea jijini Dar es Salaam.  Februari 24, 2023.

ZUIENI VITENDO VYA RUSHWA KWA KUTEKELEZA VEMA PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI-MAGU MWANZA

ZUIENI VITENDO VYA RUSHWA KWA KUTEKELEZA VEMA PROGRAMU YA TAKUKURU RAFIKI-MAGU MWANZA

Mhe. Jenista Joakim Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Wa tatu kutokakulia) amewataka TAKUKURU kujikita zaidi katika Kuzuia vitendo vya rushwa na kutekeleza vema Programu ya TAKUKURU RAFIKI kwa lengo lakuboresha huduma kwa wananchi. Pichani ni Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, kulia kwake  akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. RachelKassanda  pamoja na Watumishi wa TAKUKURU Wilaya ya Magu wakati Waziri alipokuwa wilayani humo kwenye ukaguzi wa miradi ya TASAF. TAKUKURUMwanza, Februari 22, 2023.

HIGH LEVEL CONFERENCE ON THE FIGHT AGAINST CORRUPTION IN AFRICA – BAMAKO MALI

HIGH LEVEL CONFERENCE ON THE FIGHT AGAINST CORRUPTION IN AFRICA – BAMAKO MALI

 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye, anamwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika mkutano tajwa unaofanyika Bamakonchini Mali. Mkutano huu unajumuisha viongozi wa juu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa kutoka takriban nchi 20 Barani Afrika pamoja nawataalam mbalimbali wa Umoja wa Mataifa, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika mapambano dhidi ya Rushwa. Katikapicha (katikati) ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye akiongoza kikao kazi kilichojadili kuhusu ‘ SpecificInvestigations on Corruption: What methodology to Adopt’. Kikao hiki kilichofanyika Februari 21, 2022 ni miongoni mwa vikao vidogovilivyoandaliwa kufanyika katika mkutano huo.

MAANDALIZI YA NACSAP IV

MAANDALIZI YA NACSAP IV

 Katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -  TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni,akifafanua jambo kwa Mshauri Elekezi kutoka ESRP Prof. Ernest Mallya (kulia kwake), katika kikao cha majadiliano na kupokea maoni yamaandalizi ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Nne (NACSAP IV). TAKUKURU MAKAO MAKUU. Februari 08, 2023.

Page 1 of 6 1 2 6

Taarifa kwa Umma