Ijue TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupamabana na Rushwa (TAKUKURU) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007. Sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa Sheria ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) Sura ya 329 iliyofanyiwa marrejeo mwaka 2002. Kuanzishwa kwa chombo hiki kulikuja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Mswaada wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2007 mnamo tarehe 16 Aprili, 2007. Mswaada huu ulisainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuwa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mnamo tarehe 11Juni, 2007 na ilianza kufanya kazi tarehe 1Julai, 2007.

Dhima

Kuzuia na Kupambana na Rushwa kupitia Uelimishaji Umma, Kuzuia, Utambuzi, Uchunguzi na Mashtaka, na kwa kuwashirikisha wadau ili kuifanya rushwa...

DIRA

kuwa chombo bora kinachofanya kazi zake kwa ufanisi na utimilifu huku kikiwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa...