TAKUKURU SPORTS CLUB YAREJEA NA USHINDI

Timu ya michezo ya TAKUKURU (TAKUKURU SPORTS CLUB – TSC), imerejea jijini Dodoma ikiwa na ushindi wa makombe matatu na medali ishirini na tano zilizopatikana baada ya kushiriki mashindano ya Taifa ya Mei Mosi kwa Mwaka 2025.

Zawadi hizi ni kutokana na ushiriki wa Maafisa 42 wa TAKUKURU katika michezo ya Kuvuta Kamba Wanaume; Kuvuta Kamba Wanawake; Riadha pamoja na mashindano ya mbio za kuendesha baiskeli yaliyofanyika Mkoani Singida tarehe Aprili 16,2025 hadi Aprili 29, 2025


Katika mashindano ya Mei Mosi 2025, TAKUKURU imepata ushindi katika michezo ifuatayo:-

Riadha mita 400 ambapo imekuwa mshindi wa pili na kupata medali nne za Dhahabu. Washiriki walikuwa ni (Juma Chibago, Omar Mbelwa, Marire Witimu na Ramadhan Awadhi);
Riadha Mita 100 mshindi wa pili na kupata medali ya fedha (Paul Tarimo),
Riadha Mita 100 mshindi wa pili Wazee kuanzia miaka 50 ambapo tumepata medali ya fedha (Denis Manumbu),
Riadha Mita 400 wanaume mshindi wa pili medali ya fedha (Marire Witimu),
Riadha Mita 1,500 na mita 3,000 wanaume ambapo tulikuwa mshindi wa tatu na kupata medali ya shaba (Paul Biroli)
Michezo mingine ni mashindano ya kuendesha baiskeli ambapo Chacha Ikwabe aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili na kupata medali ya fedha na mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wanawake imeweza kuvuna jumla ya medali 15 za fedha kwa kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo. Vilevile Timu ya kuvuta kamba Wanaume ilijitahidi na kufikia hatua ya robo fainali.

TAKUKURU imeshiriki katika mashindano haya ikiwa ni mara ya pili na ilijumuisha Watumishi 43 – Kuvuta Kamba Wanaume 15; Kuvuta Kamba Wanawake 13; Riadha 9; Daktari mmoja na Viongozi Watano.

Taarifa kwa Umma