Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, anashiriki Mkutano wa 15 wa Kimataifa wa Wakuu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa kwa Nchi za Jumuiya ya Madola – Kanda ya Afrika (15th Commonwealth Regional Conference of Heads of Anti-Corruption Agencies in Africa), unaofanyika Cape Town – Afrika Kusini kuanzia Mei 5 – 9, 2025.
Mkutano huu una lengo la kuimarisha ushiriki wa wadau (Taasisi za Serikali na Zisizo za Serikali), katika kuzuia na kupambana na rushwa Barani Afrika.
Kupitia mkutano huu Mkurugenzi Mkuu ametoa wasilisho kuhusu ‘INTERGRATING ANTI – CORRUPTION CONTENT INTO THE EDUCATION CURRICULUM IN TANZANIA’ , lililoangazia mafanikio ya Tanzania katika jitihada za kuzuia na kupambana na Rushwa.