Aprili 8 – 9, 2025, Bibi. Neema Mwakalyelye – Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, alishiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Mapambano Dhidi ya Rushwa (Partnerships for Anticorruption – Global Forum 2025) uliofanyika Washington DC – Marekani.
Mkutano huu umeandaliwa na kuratibiwa na Benki Kuu ya Dunia lengo likiwa ni kuangazia umuhimu wa kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wadau wa mapambano dhidi ya rushwa.
Katika Mkutano huu Naibu Mkurugenzi Mkuu ameambatana na Afisa Uchunguzi Bw. John Sang’wa kutoka Kurugenzi ya Uchunguzi.