Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa pongezi kwa TAKUKURU kwa utendaji kazi mzuri na hasa kwa kuwashirikisha vijana tangu wakiwa na umri mdogo.
Akitoa pongezi hizo Mhe. Rais Samia amesisitiza kuendelea kutoa elimu kwa vijana ili kuwajengea uadilifu na kujenga Taifa imara. “Udongo uupate ungali mbichi, ili uweze kuufinyanga” Alisema Mhe Rais.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa Mwaka 2023/2024, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila. Hafla hii ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Machi 27, 2025.