Januari 15, 2025 lilifunguwa shauri la jinai Na. 1337/2025 Jamhuri Vs ISAKA EMIL KAYUNGU na LUSESA PETER GEOCEPH katika Mahakama ya Wilaya ya Uvinza mbele ya Mheshimiwa Misana M. Majura – Hakimu Mkazi Mkuu.
Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri Amrani Buyege aliieleza mahakama kuwa Oktoba 15, 2024 Bw. Isaka Emil Kayungu ambaye ni mwajiriwa wa mkataba wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kwa kushirikiana na LUSESA PETER GEOCEPH ambaye ni Wakala wa Huduma za Kifedha ya Mpesa, Tigo pesa na Airtel Money, waliomba na kupokea rushwa ya shilingi 609,500/= kutoka kwa mmoja wa Mfugaji Uvinza ili waweze kuziachia Ng’ombe zake 65 zilizokamatwa kwa kosa la kuvuka Reli katika eneo lisiloruhusiwa kisheria.
Washtakiwa wote wawili walikana kuhusika na makosa hayo.
Washtakiwa wote walikidhi masharti ya dhamana na mahakama iliwapa dhamana.
Shauri limepangwa kusikilizwa tena mahakamani Februari 11, 2025