Januari 16, 2025, Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) baina ya TAKUKURU, TSA na ZAECA (wa pili hadi wa nne kutoka kushoto – walioketi), ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin F. Chalamila, Skauti Mkuu wa TSA Bw. Rashid K. Mchatta na Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Bw. Ali Abdala Ali, wamefanya kikao kazi wakiwa na baadhi ya watendaji wa Taasisi hizo.
Kikao hicho kilichojadili utekelezaji wa ushirikiano huo kilifanyika katika ofisi za TAKUKURU Ilala mkoani DarΒ es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo:
π Imejadili Taarifa ya Utekelezaji wa MoU
π Imepitisha Mpango Kazi wa utekelezaji wa MoU na pia
π Imepitisha Maboresho ya Mwongozo wa Mafunzo kwa Wawezeshaji Kufundisha Vijana wa Skauti kuhusu Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi.