“Ninaipongeza Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, kuanzisha Midahalo kwa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu.
Ninajivunia midahalo hiyo ambayo kwa kipekee inafanyika kwenye Mkoa wa Dodoma. Mwaka 2024 nilishiriki kwenye mdahalo na nilishuhudia vijana wazalendo wakitoa hoja za msingi na elimu ya mapambano dhidi Rushwa, hivyo ninaomba mwaka huu nawe ushiriki ili ujione vijana wazalendo wanavyotoa mawazo na michango katika kuzuia vitendo vya rushwa nchini”
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule alipotembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila.
TAKUKURU -DODOMA, Januari 8, 2025.