TAKUKURU yasaidia watoto njiti Hospitali ya Mount Meru Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amekabidhi dawa na vifaa tiba, kwa ajili ya watoto njiti, vyenye thamani ya zaidi ya Sh. 15,000,000.

Chalamila ametoa wito kwa Watanzania kushiriki katika kuchangia katika sekta ya afya, haswa amehimiza umuhimu wa kuchangia damu hospitalini.

Hii ni picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa TAKUKURU, baada ya kutembelea na kukabidhi Dawa na Vifaa Tiba kwa Watoto Njiti. TAKUKURU Arusha Desemba 19, 2024