Mnamo Disemba 2, 2024 Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo Bi. Happy Geofrey alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ubungo na kufunguliwa Shauri la Uhujumu Uchumi namba 33707/2024.
Katika Shauri hili Bi. Happy anashtakiwa kwa kufanya ubadhirifu wa fedha kiasi cha Tsh. 69,939,500/= ikiwa ni mapato ya ada ya taka na ulinzi shirikishi kupitia mfumo wa POS, kinyume na Kifungu cha 28(1) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka
2022.
Pia ameshtakiwa kwa kosa la kutumia madaraka yake vibaya Kinyume na Kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.
Mashtaka haya yalisomwa na waendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili
Florida Mutalemwa na Sophia Nyanda, mbele ya Mhe Tumsifu Gideon Barnabas, Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Ubungo
Kesi hiyo itakuja tena Mahakamani tarehe 17/12/2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.