Mkurugenzi wa Uchunguzi TAKUKURU Bw. Simon Maembe akiwa pamoja na Bw. Dennis Lekayo kutoka Kurugenzi ya Uzuiaji Rushwa, wamewasilisha Maoni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Mapambano Dhidi ya Rushwa – UNCAC.
Hii ni katika kikao cha ‘Second Resumed Fifteenth Session of UNCAC’ kinachoendelea Vienna Austria kuanzia Novemba 4 hadi 8, 2024.
Kupitia wasilisho hilo Bw. Maembe amezungumzia umuhimu wa kuandaa ripoti za kina baada ya mapitio ya nchi, umuhimu wa majadiliano ya ana kwa ana kama njia ya kubadilishana taarifa na pia umuhimu wa matumizi ya “templates” maalum za kuwasilisha taarifa ili kuhakikisha uwazi na ufanisi katika mapambano dhidi ya rushwa.
Wasilisho hilo pia limeeleza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kutekeleza misingi ya Mkataba wa Kimataifa wa Mapambano Dhidi ya Rushwa (UNCAC).