Viongozi watatu wa TAKUKURU – DAHRM Bw Ayoub Akida, RBC SHINYANGA – Donassian Kessy na RBC KATAVI Bw. Faustine Maijo,
ni miongoni washiriki wa Mission ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC (SADC Electoral Observers Mission – SEOM) kutoka Tanzania.
Mission hii ni kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi wa Bunge la Mauritius utakaofanyika Novemba 10, 2024.
Waangalizi wa Uchaguzi huu wanatoka nchi 9 wanachama wa SADC ambazo ni Botswana, Malawi, Zambia, Eswatini, Afrika ya Kusini, Namibia, Zimbabwe, Msumbiji pamoja na Tanzania.
Kiongozi wa SADC anayesimamia Uchaguzi wa Mauritius kwa niaba ya Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC – Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan – Rais wa JMT ni Mheshimiwa Mohammed Othman Chande, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania.