Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, amehitimisha Mafunzo ya Awali ya Uchunguzi kwa Waajiriwa wapya wa TAKUKURU na kusema kuwa mapambano dhidi ya Rushwa si jukumu la TAKUKURU Pekee.
Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika Oktoba 26, 2024 katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi, Mhe Waziri Mkuu amesema kila Mtanzania anapaswa kushiriki kikamilifu kusimamia maadili na kupinga vitendo vya Rushwa.