Bw. Crispin Francis Chalamila, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU amehudhuria Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika Oktoba 21, 2024 jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alitoa Taarifa ya Utendaji wa Wizara yake kwa kipindi cha kuanzia Aprili – Septemba 2024, taarifa ambayo inajumuisha Taarifa ya Utendaji wa TAKUKURU.