Mkurugenzi Mkuu amewashukuru nchi wanachama kwa ushirikiano na uungaji mkono wa juhudi za kikanda za Kuzuia na Kupambana na Rushwa na amempongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kupambana na Rushwa ya Zambia, Monica Chipanta Mwansa (ambaye ni mwenyekiti aliyemaliza muda wake), kwa maendeleo yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na hususan katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa SADC wa Kupambana na Rushwa (2023-2027), ambao unatekeleza malengo ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC.
Wakuu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa ukanda wa SADC pamoja na Viongozi na wajumbe mbalimbali kutoka katika mamlaka hizo za Nchi 14 wanachama waliohudhuria mkutano huo
Mkutano huu wa siku tatu umehudhuriwa na nchi wanachama 14 na umefunguliwa rasmi na
Kamishna Francis Chilinga, kutoka Wizara ya Sheria ya Zambia.
Tanzania inahudumu kama Mwenyekiti wa SACC kwa Mwaka 2024/ 2025 ikiwa ni mara ya pili baada ya kuhudumu kwa nafasi hiyo Mwaka 2017/2018 – mwaka ambao kamati hiyo ya SACC ilizinduliwa.
Wakuu wa Mamlaka za Kupambana na Rushwa ukanda wa SADC pamoja na Viongozi na wajumbe mbalimbali kutoka katika mamlaka hizo za Nchi 14 wanachama waliohudhuria mkutano huo