Kikao cha Menejimenti kinachoundwa na Taasisi tatu (UTATU) ambazo ni TAKUKURU, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Jeshi la Polisi kupitia Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kimefanyika Oktoba 8, 2024 jijini Dodoma.
Kikao hicho kilichofunguliwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini – DCI Bw. Ramadhani Kingai, kinafanyika kwa lengo la kufanya tathmini ya kazi zilizotekelezwa kwa mwaka na kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano baina ya Taasisi hizo zinazohusika na Uchunguzi na Uendeshaji wa wa Mashtaka.
Akizungumza DCI Kingai amesema ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizo umeendelea kuleta matokeo chanya kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki zao kwa wakati.
Katika hatua nyingine Bw Crispin Francis Chalamila, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakati wa ufunguzi wa kikao hicho amewashukuru DPP na DCI kwa kumpokea na kumjumuisha kwenye UTATU.
Mkurugenzi Mkuu ameeleza pia kwamba umoja huu unarahisisha utekelezaji wa majukumu waliyopewa dhamana ya kuyasimamia.
BIBI. NEEMA MWAKALYELYE NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU AKITOA NENO LA UKARIBISHO NA UTAMBULISHO WAKATI WA UFUNGUZI WA KIKAO HICHO
Kikao hiki cha UTATU kinaendelea kwa siku tatu jijini Dodoma ambapo kesho kinawajumuisha wate daji wakuu wa Mikoa kutoka taasisi hizi tatu.