Kaimu Mkurugenzi Mkuu amepokea ugeni kutoka Kitengo cha Maadili – Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini ukiongozwa na Bw. Richelieu Lomax na Bw. Leonard Nkurunziza. Viongozi hawa walifika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na TAKUKURU ambapo kwa Pamoja wamekubaliana kushirikiana katika Nyanja za Uzuiaji Rushwa, kuwajengea uwezo maafisa uchunguzi pamoja na utoaji wa misaada ya kiufundi.