TAKUKURU kwa mara ya kwanza, imeungana na Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Kimataifa nchini Msumbiji, kupitia utaratibu wa ‘SADC ELECTION ORGANIZATION MISSION – “SEOM”.
Katika picha ni Timu ya Waangalizi hao wakiwa na kiongozi wa Kamisheni inayosimamia uchaguzi Msumbiji – “CNE” Provience ya Gaza.
Mhe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Aman Abeid Karume ndiye mkuu wa Mission hiyo akimwakilisha Mwenyekiti wa SEOM ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dr Samia Suluhu Hassan.
Awali Waangalizi walipata mafunzo ya siku 4 (28.09.- 01.10.2024) na kisha kuanza kazi ya uangalizi wa Kampeni, Usambazaji wa vifaa vya kupigia kura, Upigaji wa kura, Uhesabuji wa kura, Upokelewaji wa kura kutoka vituoni kwenda Makao Makuu ya nchi hiyo Maputo pamoja na Kupata maoni ya wadau baada ya upigwaji wa kura.
Nchi ya Msumbiji imefanya uchaguzi wake mkuu Oktoba 9, 2024 ambapo uchaguzi ilihusisha Rais, Wabunge na Wawakilishi wa majimbo.