Viongozi wa TAKUKURU Kurugenzi ya Uchunguzi Bw. Thobias Ndaro na Alexander Kuhanda, wanahudhuria mafunzo maalum yanayoendeshwa na SADC nchini Botswana kuanzia Oktoba 17-20, 2024.
Mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 30, 2024 ambapo Tanzania inaungana na nchi nyingine mwanachama wa SADC katika zoezi hilo la uangalizi.
Pamoja na Tanzania, nchi nyingine zilizotuma waangalizi ni Zambia, Malawi, DRC, South Africa, Zimbabwe, Namibia, Msumbiji, Eswatin na Lesotho