Mkurugenzi Mkuu pia alipata wasaa wa kumtembelea Katibu Mtendaji wa Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri kuhusu masuala ya Rushwa – AUABC Bibi. Charity Nchimunya.
Mkurugenzi Mkuu ambaye amefika AUABC Septemba 13, 2024 kwa lengo la kujitambulisha, ameshukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya AUABC na TAKUKURU na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo na kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa – AUCPCC.