Christian Nyakizee, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni ni miongoni mwa washiriki 19 waliopata mafunzo katika Chuo cha Taifa cha Kupambana na Rushwa – Cairo nchini Misri, kuanzia Oktoba 7 hadi 10, 2024.
Kupitia mafuzo hayo washiriki wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza mbinu za kuzuia na kupambana na vitendo vya Rushwa.
Vilevile, wamejifunza namna nchi ya Misri inavyotekeleza Mikakati ya Kuzuia Rushwa na walivyofanikiwa kupambana na vitendo hivyo kupitia chunguzi na mashtaka yaliyowahi kufanyika (case studies) dhidi ya watuhumiwa.
Pia wamepata uelewa wa namna Misri walivyofanikiwa kukamata na kutaifisha mali za watuhumiwa zilizopatikana kwa njia za uhalifu ikiwemo Rushwa.