Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw Crispin Francis Chalamila amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa ushirikiano na jitihada anazozifanya katika kuzuia na kupambana na Rushwa katika Mkoa wa Arusha.
Mkurugenzi Mkuu ameyasema hayo Septemba 13, 2024 alipofika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa ajili ya salamu na mazungumzo.
Katika mazungumzo yake, Mhe. Makonda amesema TAKUKURU Mkoa wa Arusha wanafanya kazi nzuri na anatamani mkoa wake huo uwe ni mkoa wa mfano wa kuigwa katika kudhibiti vitendo vya rushwa.