MGENI RASMI UTATU

PROFESA, Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, amezipongeza TAKUKURU, NPS na Ofisi ya DCI kwa kuunda umoja unaojulikana kama UTATU ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya uchunguzi, upekekezi wa makosa ya jinai pamoja na uendeshaji wa mashtaka.

Hayo ameyasema jijini Dodoma Oktoba 9, 2024 wakati akifungua rasmi kikao cha Viongozi wa ofisi hizo ngazi ya Makao Makuu na mikoa, chenye lengo la kutathmini utekelezaji wa malengo waliyojiwekea kwa mwaka mmoja.

Aidha, amezitaka Ofisi hizo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia misingi ya haki ili kuhakikisha Amani, Utulivu na Umoja vinatamalaki kwa maendeleo ya nchi yetu.

Taarifa kwa Umma