Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, amemtembelea Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Khamis Mussa Omar Septemba 23, 2024.
Akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu, Balozi Omar ameipongeza TAKUKURU kwa jitihada inazozifanya katika kuzuia na kupambana na rushwa na kusisitiza TAKUKURU kutumia vema fursa ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na ya China kwani kuna mambo mengi ya kujifunza.
Mkurugenzi Mkuu yuko China kuhudhuria ‘The 5th GlobE Network Meeting’ inayofanyika Beijing China Septemba 24 – 27, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine atawasilisha mada kuhusu Mfumo wa Sheria wa Tanzania kwenye Mapambano dhidi ya Rushwa.