Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeibuka kidedea kwa kuwa moja ya Taasisi 10 za Umma zinazowajibika zaidi kwa kujibu hoja zinazoibuliwa kupitia majukwaa ya kidijitali na kuchukua hatua.Kupitia shindano la ‘Stories of Change’ linaloendeshwa na JamiiForums kwa kushirikiana na wadau wa kimkakati, TAKUKURU imetambulika kama moja ya taasisi iliyo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa kero mbalimbali zinatatuliwa katika jamii.Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKRU, Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Bi Sabina Seja alisema taasisi hiyo inafanya kazi na wadau ikiwemo JamiiForums kupitia majukwaa yake ambayo taarifa mbalimbali huchapishwa na wananchi.
“Kupitia forums [majukwaa] ya namna hii TAKUKURU inapata taarifa na kuzifanyia kazi. Tuzo hii tumeipata kwa kuwa TAKUKURU imekuwa ikichukua hatua kwa kero zinazotolewa ….kwa maana hiyo inachangia mapambano dhidi ya rushwa”.