Septemba 26, 2024 Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa baadhi ya Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanaoshiriki Mkutano wa GlobE Network unaoendelea Jijini Beijing China kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya TAKUKURU na Mamlaka hizo.
Viongozi aliokutana nao ni kutoka National Commission of Supervision ya China Beijing (NCS), Independent Commission Against Corruption (ICAC) ya China Hong Kong na National Prosecutions Authority – (NPA) ya Afrika Kusini.
Kwa ujumla wake viongozi hao wamepongeza jitihada za TAKUKURU katika Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na ushirikiano walionao Kikanda na Kimataifa.