Septemba 24, 2024 Ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) umetembelea ofisi za TAKUKURU Upanga jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendeleza ushirikiano.
Ujumbe huo uliongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Phan Dinh Trac wakiambata na Balozi wa Vietnam hapa nchini – VuThanh Huyen.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Naibu Mkurugenzi Mkuu Bibi Neema Mwakalyelye ameueleza ujumbe huo namna TAKUKURU inavyotekeleza majukumu yake na namna inavyoshirikiana na wadau wa kitaifa na kimataifa katika kuzuia na kupambana na rushwa.
Bibi. Neema ameushukuru Ujumbe huo kwa kutembelea TAKUKURU.
Ujumbe huo umepongeza jitihada za TAKUKURU na Serikali kwa ujumla katika kuzuia na kupambana na Rushwa.