Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila ameeleza namna ambavyo Mfumo wa Sheria na Kitaasisi nchini Tanzania unawezesha Mapambano Dhidi ya Rushwa kufanikiwa.
Ameyasema hayo akiwasilisha mada kuhusu ‘ANTI CORRUPTION AND INSTITUTIONAL LEGAL FRAME WORK IN TANZANIA’ kwenye Kongamano la Wakuu wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa wanaoshiriki ‘The 5th Global Operational Network of Anti Corruption Law Enforcement Authorities – GlobE Network’.
Mkurugenzi Mkuu amesema Serikali ya Tanzania imekuwa ikipambana na Rushwa kwa kuimarisha mifumo ya sheria na ya kitaasisi ikiwemo kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama Kuu inayoshughulikia masuala ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Kongamano hili linahudhuriwa na Mamlaka 219 za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi 121 Duniani – Tanzania ikiwa ni kati ya Nchi 70 zilizopewa fursa ya kutoa wasilisho.
Mtandao wa GlobE ulianzishwa 2021 kwa lengo la kubadilishana taarifa, uzoefu na utaalamu katika mapambano dhidi ya Rushwa na TAKUKURU ilijiunga Mwaka 2022.