Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni akiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester A. Mwakitalu, wamefanya ziara ya kikazi na kutembelea ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Katavi ambapo pia wamefanya kikao kazi na watumishi.
Kwa pamoja, viongozi hawa ambao wanashirikiana kwa karibu katika utendaji kazi, wamesisitiza ushirikiano huo utekelezwe pia katika ngazi za mikoa na wilaya, uadilifu, kupendana pamoja na matumuzi ya mifumo katika kutekeleza majukumu ya Taasisi.