THE 8th ICAC SYMPOSIUM

Mkutano Mkuu wa 8 unaojumuisha viongozi na wadau zaidi ya 500 kutoka Mamlaka za Kupambana na Rushwa Duniani umefanyika jijini Hongkong China, ajenda kuu ikiwa ni kubadilishana uzoefu na kujadili mbinu mpya za mapambano dhidi ya rushwa duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amehudhuria mkutano huo unaofanyika chini ya kaulimbiu isemayo: “Charting a New Path to Combat Corruption” na kuratibiwa na Independent Commission Against Corruption – ICAC. Mkutano huu unaofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 11 wa Shirikisho la Kimataifa la Mamlaka za Kupambana na Rushwa – IAACA, uliofunguliwa Mei 22 na kuhitimishwa Mei 24, 2024. Katika hatua nyingine, Mei 24, 2024, Mkurugenzi Mkuu amekutana na kufanya kikao cha kuimarisha mashirikiano na mahusiano na Bw. Kenneth Wong, ambaye ni Director of International Cooperation and Corporate Services – ICAC.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kukuza mashirikiano kati ya taasisi hizi mbili ambapo pamoja na mambo mengine, wemejadili kuhusu namna bora ya kushirikiana katika mafunzo kupitia Anti – Corruption Academy ambayo ICAC wameianzisha tangu Mwezi Februari, 2023.

Taarifa kwa Umma