
Bw. Mkomi ameyasema haya wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Kujadili Mkakati wa Kudhibiti Rushwa ya Ngono Mahala pa Kazi iliyofanyika Julai 2, 2024 jijini Dodoma.
Pia amewataka washiriki wa warsha hiyo ambao wengi wao ni Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka Wizara na Taasisi za Serikali, kutengeneza Mkakati madhubuti wa kudhibiti vitendo vya rushwa ya ngono kwenye maeneo yao unaotekelezeka na wenye kuleta tija kwa Taifa.

Mkurugenzi Mkuu amesema katika eneo la utafiti, TAKUKURU kwa kushirikiana na Taasisi ya Women Fund Tanzania Trust – WFT ilifanya utafiti katika Vyuo Vikuu saba (7), na katika sekta ya elimu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kwa malengo mahsusi ya Kubaini uwapo, sababu, mbinu na wahusika wa vitendo vya rushwa ya ngono.
Pamoja TAKUKURU wadau wengine ambao WSP, TAMWA nao walifanya utafiti katika eneo hili la rushwa ya ngono.