Mahakama ya Wilaya Biharamulo imewatia hatiani wazabuni wawili Bw Salanga Mayenga na Bw Vedasto Kiporoka.
Washtakiwa wametiwa hatiani na kuaamriwa walipe faini ya shilingi milioni moja au kutumikia kifungo cha Mwaka Mmoja kwa kosa la Hongo k/f 15 (1) (a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya Mwaka 2022.
Hukumu hiyo dhidi ya washtakiwa Salanga Mayenga na Vedasto Kiporoka katika Shauri Namba 5943/2024, imetolewa na Mhe Flora Ndare Hakimu Mahakama ya Wilaya ya Biharamulo Aprili 9, 2024.
Kwamba kati ya Mwezi Mei na Juni 2023, washtakiwa walijipatia manufaa isivyo stahili ya hongo ya Shilingi 3,278,700/= katika manunuzi ya vifaa vya umeme kwa kuzidisha malipo ya bei ya vifaa kwenye mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Kikomakoma mpya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo.
Washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru na mahakama.