Mahakama ya Wilaya Muleba imemhukumu Bw. Alexander Mathias Rugema – Mkusanya Mapato ya Hamshauri ya Wilaya ya Muleba kwa njia ya POS.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi 500,000/- au jela miaka miwili kwa kujipatia manufaa ya shilingi 2,074,500/= kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.
Hukumu hiyo dhidi ya Bw Alexander Mathias Rugema katika Kesi ya Jinai namba 9168/2024 imetolewa chini ya Mhe. Lilian Mwambeleko – Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Muleba Aprili 8, 2024
Kwamba mshtakiwa akiwa Mkusanya Mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa njia ya POS, alishtakiwa kwa kosa la Hongo na kujipatia manufaa yasiyostahili wakati wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali, hivyo kufanya upotevu wa shilingi 2,074,500/= mali ya Halmashauri ya Muleba.
Mshtakiwa amelipa faini mahakamani ya sh 500,000/= na kutanguliza sh 810,000/= kama fedha alizojinufaisha nazo kwa kujutia kosa lake, na mahakama imemuamuru kukamilisha fedha zote zilizobaki ndani ya miezi mitatu na kuachiwa huru.