Shauri la Uhujumu Uchumi namba 9069/2024 limefunguliwa Aprili 8, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Ilala mbele ya Mhe. Aneth Nyenyema-Hakimu Mkazi Mwandamizi,
ambapo washtakiwa:
1.Sefania Adam Mwanja– Mweka Hazina kikundi cha Afya Jamii,
2.Eric Isack Gabriel– Mtaalamu wa Maabara,
3.Sabina William Ndasi– Mtendaji wa Mtaa wa Kitinye na
4.Jacob Chacha Mwita-Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kitinye,
wamesomewa jumla ya mashtaka 18 ya Kughushi, Uhujumu Uchumi na Utakatishaji Fedha Haramu, kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022 ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi sura 200 marejeo ya 2022 na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji fedha, Sura ya 423 marejeo ya Mwaka 2022.
Washtakiwa wote wamekana makosa yao na kupelekwa rumande baada ya kutotimiza vigezo vya dhamana kwa mshtakiwa namba 2-4.
Aidha, Mshtakiwa wa kwanza hajapewa dhamana kwa kuwa ana shtaka la utakatishaji fedha ambalo halina dhamana kisheria.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 22, 2024 kwa ajili ya kusoma hoja za awali.
Msingi wa shauri hili ni udanganyifu katika uundwaji wa kikundi ambacho kilipewa mkopo wa shilingi milioni 100.