Machi 28, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, imefunguliwa kesi ya jinai dhidi ya Bi Mery James Numbi, kwa kosa la kuomba na kupokea Rushwa kinyume na Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (cap 329 Re 2022).
Mshtakiwa akiwa Mtendaji wa Kijiji cha Lupembe cha Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, aliomba rushwa kiasi cha shilingi 200,000 kutoka kwa Bi Irine Justine na kupokea kiasi cha shilingi 200,000 ili asimchukulie hatua za kisheria kwa mtoto wake kutopelekwa shule.
Mshtakiwa alisomewa mashtaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe na Catheline J Kayombo ambapo alikana makosa yote na kupewa dhamana.
Shauri limepangwa kusikilizwa tena Aprili 17, 2024.