Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu Bw. RAMADHANI RASHID MSANGI ambaye ni Mshauri wa Wafanyabiashara mwajiriwa wa Chama cha wenye viwanda na kilimo Mkoa wa Manyara (Bussines consultant -TCCIA Manyara).
Mshtakiwa ameamriwa kulipa faini kiasi cha shilingi 900,000/= au kwenda jela miaka mitatu, kwa kosa la kughushi nyaraka za malipo.
Hukumu hiyo dhidi ya Ramadhani Rashid Msangi katika shauri la uhujumu uchumi Na. 05/2023, imetolewa chini ya Mhe. Martin Massao, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Manyara Machi 22, 2024.
Mshtakiwa alighushi nyaraka mbali mbali katika marejesho yake kuonesha kuwa alihudhuria na kuendesha mafunzo ya wajasiriamali yaliyofanyika wilayani Hana’ng kwa kipindi cha Mwezi Februari na Juni Mwaka 2018 na kwamba alitumia kiasi cha shilingi 6,695,000/= kugharamia posho ya chakula , ukumbi na nauli kwa waliodaiwa kushiriki mafunzo hayo – huku akijua taarifa hizo hazikuwa sahihi.
Mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na mahakama