AFISA MTENDAJI ATIWA HATIANI KWA KUOMBA NA KUPOKEA HONGO
Mahakama ya Wilaya ya Kyela imemhukumu Bw. Edestus Clemence Ndunguru – Afisa Mtendaji na Mkazi wa Kata ya Lusungo, kulipa faini ya Shilingi 500,000/= au kwenda jela miaka mitatu, kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo ya Shilingi 200,000/=.
Hukumu hiyo dhidi ya Edestus Clemence Ndunguru katika shauri la jinai Na. 2946/2024, imetolewa chini ya Mhe. A.S Njau – Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kyela, Machi 5, 2024.
Mshtakiwa huyo alishawishi,
kuomba na kupokea hongo ya Shilingi 200,000/= ili amsaidie mwananchi kuongea na askari polisi waweze kumpa dhamana katika Kituo cha Polisi Ipinda Wilayani Kyela.
Mshtakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na Mahakama imemuamuru mshtakiwa arejeshe kiasi cha 200,000/= alichopokea toka kwa mwananchi.