Machi 5, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Hai mbele ya Mhe. Julieth Mawole Hakimu Mkazi Mwandamizi, limeamuriwa Shauri la Jinai namba 112/2023 Jamhuri dhidi ya BENSON NICONORY MASSAWE kwa kumtia hatiani kwa kosa la Wizi wa Kuaminiwa k/f 258 (1), (2) (a) na 273 (b) Cha Penal Code Cap 16 R.E 2019.
Kwamba mshtakiwa akiwa na cheo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Chakula Shule ya Msingi Nkoraya, Wilaya ya Hai, Mkoa Kilimanjaro, akiwa ameaminiwa na wazazi kwa ajili ya kununua chakula cha wanafunzi na kulipa mishahara ya wapishi, alizitumia jumla ya shilingi 1,005,000/= kwa matumizi yake binafsi.
Mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo baada ya kusomewa hati ya mashitaka na hoja za awali.
Mshitakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa kulipa fedha zote alizoisababishia hasara Shule ya Msingi Nkoraya kiasi cha shilingi 1,005,000/= na kutokufanya makosa kwa kipindi cha miezi mitatu.