Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni, anahudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa barani Afrika, unaofanyika Algiers – Algeria, Machi 5 – 6, 2024.
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizoridhia na kusaini Mkataba wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (African Union Convention on Preventing and Combating Corruption – AUCPCC) uliosainiwa Julai 11, 2003 jijini Maputo, Msumbiji.
Kupitia Mkataba huu, Mwaka 2011 lilianzishwa Shirikisho la Mamlaka za Kupambana na Rushwa Afrika (Association of Anti – Corruption Authorities in Africa – AAACA), likiwa na lengo la kuhimiza nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kusaini na kuridhia utekelezaji wa AUCPCC.
Tanzania (TAKUKURU), ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya AAACA inayowakilisha Mamlaka za Kupambana na Rushwa ukanda wa Afrika Mashariki katika kamati hiyo.