KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MISSENYI- MKOA WA KAGERA.
Februari 28, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Missenyi mbele ya Mhe. Yohana Myombo, Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Missenyi, imeamriwa kesi ya Rushwa Na 05/2023.
Kesi hii ni ya Jamhuri dhidi ya Bi Rehema Mdaki ambaye alishitakiwa kwa kosa la Kutoa HONGO ya TZS 8,000,000/- kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya 2022, kwa lengo la kuwashawishi maafisa wa mpakani TRA, Kilimo na Mionzi, kuachia mzigo wa madawa ya Kilimo (pesticides) kutoka Uganda wenye thamani inayokadiriwa kuwa TZS Milioni thelathini kwa kukosa vibali vya kuagiza na kupitisha mpakani kuingia Tanzania.
Upande wa Jamhuri (PCCB) uliwakilishwa na Wakili. Kelvin Murusuri na Sospeter Joseph kwa kusikiliza mashahidi sita na vielelezo viwili wakati upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Mawakili watatu Wakili Fahady, Binamungu na Fredy wakiwa na mashahidi watatu na kielelezo kimoja
Baada ya Mahakama kusikiliza pande zote, iliridhika kutendwa kwa kosa la Kutoa Hongo na kumtia Hatiani.
Mahakama imemhukumu mshtakiwa kulipa faini ya TZS Milioni Moja au kwenda jela miaka mitatu
Aidha Mahakama pia imeridhia na kutoa Order ya kutaifisha fedha Milioni Nane zilizokamatwa kwenye tukio kupitia maombi ya Wakili Murusuri maana zilikusudiwa kutolewa kama hongo hivyo ni fedha haramu za uhalifu.
Mahakama imeelekeza fedha hizo kuwa *Mali ya Umma na ziwekwe kwenye akaunti ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.