Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mwakalyelye, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu amepokea ugeni wa viongozi na washiriki wa mafunzo ya uongozi, kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC). Ugeni huu ulifika TAKUKURU Februari 21, 2024 kwa lengo la kujifunza kuhusu majukumu ya TAKUKURU kama moja ya chombo cha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na namna inavyodhibiti Rushwa katika jamii inayoishi mipakani. Vilevile, wageni hawa walitembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya TAKUKURU MAKAO MAKUU.
Kikao kazi pamoja na wageni hawa kilifanyila katika ukumbi wa jengo la TAKWIMU lililoko jirani na ujenzi wa ofisi ya Makao Makuu.