MKUSANYA USHURU AHUKUMIWA KWA KUTOA HONGO.
Februari 15, 2024 kesi namba cc 3998/2024 imeamuliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ambapo imemtia hatiani Bw. MOSES JOHN ZIMBA (Mkusanya Ushuru Stendi ya Mabasi Bunju), kwa kosa la Kuomba na Kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 RE 2019].
Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya mshtakiwa kukiri kosa lake.
Ifahamike kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la kuomba rushwa ya kiasi cha shilingi 150,000/ kutoka kwa kondakta wa daladala ili ampunguzie kulipa fine ya shilingi 300,000 kwa kosa la kutolipia ushuru katika stendi ya mabasi Bunju.
Baada ya Mahakama kumtia hatiani imemhukumu mshtakiwa kulipa faini ya shilingi laki tano (500,000) au kifungo cha miaka miwili (2) gerezani.
Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Mheshimiwa Janeth Kaluyenda na mshtakiwa amelipa faini.