Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni amepokea ugeni wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo Kariba, aliyefika TAKUKURU Februari 12, 2024 kwa lengo la kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika uandaaji na uendeshaji wa mafunzo mbalimbali ya watumishi wa Umma – hususan katika kuwaandaa kuwa viongozi. Katika ziara hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu Singo alipata maelezo kuhusu uendeshaji wa mafunzo ndani ya TAKUKURU ambapo naye alieleza uzoefu wake katika eneo hilo. Katika ziara hii Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Singo aliambatana na watendaji wawili wa Taasisi ya Uongozi Bw. Emmanuel Tessua na Bi Kanisia Ignasi. Baada ya majadiliano, Mkurugenzi Mkuu alimkabidhi Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi zawadi za kumbukumbu.