KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA UYUI – TABORA


Mnamo Februari 9, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Uyui, mbele ya Mh. Tausi Mongi, imefunguliwa kesi ya jinai (Criminal case No. 20240209000003354) Jamhuri dhidi ya GEORGE FICHA MANYAMA (Mwenyekiti wa Chama cha Wauza Mikaa – UWAMUKU – Tabora). Kesi imefunguliwa na waendesha Mashitaka wa TAKUKURU – Annifa Kapinga & Mwanaidi Mbuguni, ambapo mshtakiwa anakabiliwa na makosa chini ya kf cha 15 (1) (a) & (b) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2022.

Mshitakiwa, Desemba 2022 kupitia simu yake ya mkononi, alishawishi na kujipatia hongo ya fedha za kitanzania shilingi laki tatu (Tzs. 300,000/= kutoka kwa mwananchi (Jina limehifadhiwa), ili kutomchukulia hatua za kisheria kwa kutokufuata matakwa ya usafirishaji wa mkaa katika ujazo unaopaswa kisheria.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake amekana mashitaka yote.

Mshtakiwa yuko mahabusu kwani hakutimiza vigezo na masharti ya dhamana.

Shauri limepangwa kurudi kwa usikilizwaji Februari 23, 2024.

Taarifa kwa Umma