Februari 7, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh Lilian Mwambeleko, imeamriwa kesi ya Jinai namba 09/2023, Jamhuri dhidi ya Archileus Anatory Rutayungulwa– Mkusanyaji wa mapato kwa njia ya POS na mwajiriwa wa Halmashauri ya Muleba.
Huyu alishtakiwa kwa kosa la kutotii wajibu wa kisheria wa kukusanya maduhuri ya Serikali na kuweka katika akaunti ya Halmashauri ya Muleba na hivyo kufanya upotevu wa TZS 3,116,300/- mali ya Halmashauri ya Muleba.
Kosa hili ni kinyume na kif cha 123 cha Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022.
Kesi hii iliongozwa na Wakili Kelvin Murusurikutika TAKUKURU.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kukiri kosa lake mwenyewe na kuthibitisha kuwa amesharejesha fedha zote TZS 3,116,000/- kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba.
Mahakama imempatia adhabu ya kutotenda kosa lolote kwa miezi sita na kifungo cha nje kwa kuzingatia kuwa amekiri kosa lake na kurejesha fedha za umma.