Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni amepokea ugeni wa Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal, aliyemtembelea ofisini kwake – PCCB HOUSE Upanga Dar Es Salaam Februari 9, 2024.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hawa wamejadili kuhusu umuhimu wa Tanzania na Algeria kushirikiana katika jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa katika nchi zao ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashirikiano ya kikazi na kusaini Mktaba wa Ushirikiano wa kikazi kati ya TAKUKURU na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa ya Algeria.